×

MUHIDIN MICHUZI's video: WIZARA YA ARDHI YABAINI VYANZO VIKUU NANE VYA MIGOGORO YA ARDHI YAJIPANGA KUITATUA

@WIZARA YA ARDHI YABAINI VYANZO VIKUU NANE VYA MIGOGORO YA ARDHI, YAJIPANGA KUITATUA
MIRATHI yatajwa kuchangia migogoro ya Ardhi ambapo hoja 12 ziliibuliwa sawa na asilimia 3.1% migogoro iliyotolewa uamuzi na mahakama au mamlaka nyinyinge ambapo hoja 65 ziliibuliwa sawa na asilimia 16.6 na changamoto za urasimishaji ambapo hoja 29 ziliibuliwa sawa na asilimia 7.4% Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt.Allan Kijazi amesema kupitia kamati aliyoiunda ya kutatua migogoro ya Ardhi jijini Dar es Salaam imebaini vyanzo vikuu nane vya migogoro ikiwemo uvamizi, kughushi nyaraka na utapeli. Dkt. kijazi ameyasema hayo leo Septemba 2, 2022jijini Dar es Salaam wakati akitoa taarifa ya matokeo ya ripoti iliyowasilishwa kwake na kamati ya wataalamu, ambapo amesema Mnamo tarehe 25 Julai, 2022 aliunda Kamati ya Wataalam wa Wizara na Mkoa wa Dar es Salaam kwa ajili ya kupokea na kusikiliza malalamiko ya wananchi kwa lengo la kuyapatia ufumbuzi. Ameongeza kuwa vyanzo vya migogoro vilivyobainishwa ni pamoja na uwepo wa milki pandikizi za ardhi ambapo hoja 13 ziliibuliwa sawa na asilimia 3.3%,uvamizi wa maeneo yenye milki za watu wengine ambapo hoja 99 ziliibuliwa sawa na asilimia 25% ,kughushi nyaraka ambapo hoja 16 ziliibuliwa sawa na asilimia 4.1% madai ya fidia ambapo hoja 62 ziliibuliwa sawa na asilimia 15.9%,uelewa mdogo wa taratibu za ardhi na masuala ya mikataba ambapo hoja 95 ziliibuliwa sawa na asilimia 24.3%. Aidha,Dkt.Allan ameyataja masuala ya mirathi kuchangia migogoro ya Ardhi ambapo hoja 12 ziliibuliwa sawa na asilimia 3.1% migogoro iliyotolewa uamuzi na mahakama au mamlaka nyinyinge ambapo hoja 65 ziliibuliwa sawa na asilimia 16.6 na changamoto za urasimishaji ambapo hoja 29 ziliibuliwa sawa na asilimia 7.4% “Kamati hiyo ilijumuisha wataalamu kutoka vyombo vya ulinzi na usalama ili kuongeza uwazi na ufanisi katika zoezi hili,napenda kuwataarifu kuwa kamati ilianza kutekeleza zoezi hilo kuanzia agosti mosi 2022 hadi tarehe 5 Agosti, 2022” “Kamati hiyo imekamilisha uchambuzi wa masuala muhimu yaliyojitokeza na inaendelea kuratibu na kusimamia utekeleza wake hasa kwa masuala ambayo vikao vya usuluhishi, uhakiki wa uwandani, ufufuaji wa mipaka, madai ya fidia, upangaji na umilikishaji” Alisema Dkt.Kijazi.

3

0
MUHIDIN MICHUZI
Subscribers
84.6K
Total Post
1.3K
Total Views
414.8K
Avg. Views
4.8K
View Profile
This video was published on 2022-09-03 09:06:35 GMT by @MUHIDIN-MICHUZI on Youtube. MUHIDIN MICHUZI has total 84.6K subscribers on Youtube and has a total of 1.3K video.This video has received 3 Likes which are lower than the average likes that MUHIDIN MICHUZI gets . @MUHIDIN-MICHUZI receives an average views of 4.8K per video on Youtube.This video has received 0 comments which are lower than the average comments that MUHIDIN MICHUZI gets . Overall the views for this video was lower than the average for the profile.

Other post by @MUHIDIN MICHUZI