×

Bongo special tv's video: SIMBA 7-0 RUVU CHAMA AIBUKA NA HILI

@SIMBA 7-0 RUVU CHAMA AIBUKA NA HILI,
KIUNGO mshambuliaji wa Simba, Clatous Chama amefunga ‘Hat-trick’ ya tisa katika michuano ya kombe la shirikisho (ASFC) baada ya kuingia kambani mara tatu timu yake ikiibuka na ushindi wa bao 7-0. Simba wameibuka na ushindi huo dhidi ya Ruvu Shooting na kutinga hatua ya robo fainali na kuungana na Azam FC, Coastal Union, Kagera Sugar, Geita Gold,Yanga, Polisi Tanzania na Pamba. Mabao hayo yanamfanya Chama kuungana na kina Abdul Suleiman ‘Sopu”, Kinda wa Tunduru Korosho wameingia kambani mara nne, Reliants Lusajo wa Namungo, Eliya Chibula Tunduru Korosho, Meshack Abraham Kagera Sugar, Paul Peter Azam FC. Wengine waliofunga mabao hayo 'Hati-triki' ni Idd Kipagwile wa KMC alipocheka na nyavu mara tatu wakati timu yake ikiiadhibu Majimaji mabao 4-1, huku Boban Zirintunsya naye akitupia matatu, Mtibwa Sugar ilipoilaza Tunduma United mabao 7-1. Kama haitoshi naye staa wa Yanga, Heritier Makambo hakuwa mbali kuingia kwenye orodha ya wakali wa 'Hati-triki' alipoiongoza timu yake kutupia mabao 4-0 dhidi ya Ihefu huku yeye akiingia wavuni mara tatu na Fiston Mayele akihitimisha karamu ya mabao hayo. Katika mchezo wa Simba uliopigwa uwanja wa Mkapa, mbali na Chama kuingia kambani mara tatu mabao mengine yalifungwa na John Bocco (2), Jimmyson Mwanuke moja na Michael Masinda ambaye alijifunga.

2

0
Bongo special tv
Subscribers
74.4K
Total Post
279
Total Views
79.6K
Avg. Views
1.3K
View Profile
This video was published on 2022-02-17 01:24:36 GMT by @Bongo-special-tv on Youtube. Bongo special tv has total 74.4K subscribers on Youtube and has a total of 279 video.This video has received 2 Likes which are lower than the average likes that Bongo special tv gets . @Bongo-special-tv receives an average views of 1.3K per video on Youtube.This video has received 0 comments which are lower than the average comments that Bongo special tv gets . Overall the views for this video was lower than the average for the profile.

Other post by @Bongo special tv