×

Eric Gabriel's video: WAZEE VIONGOZI WA DINI NA WANA SIASA ARUMERU MH RAIS MAGUFULI

@*WAZEE, VIONGOZI WA DINI NA WANA SIASA ARUMERU MH. RAIS MAGUFULI
*WAZEE, VIONGOZI WA DINI NA WANA SIASA ARUMERU WATOA AZIMIO LA KUPONGEZA KAZI NZURI ZINAZOFANYWA NA MHE RAIS MAGUFULI * Makundi ya wazee wa mila, viongozi wa dini kwa pamoja na wanasiasa wametoa wamepitisha *AZIMIO* la pamoja kupongeza kazi nzuri zinazofanywa na Serikali ya awamu ya tano chini ya *Mhe, Rais, Dkt. John Pombe Magufuli * Wakizungumza wakati wa *Kongamano la wazee la wilaya ya Arumeru* Viongozi hao kutoka Makundi mbalimbali wamesema kazi zilizofanywa na *Mhe Rais,Dkt. Magufuli* kwa kipindi kifupi tangu aingie madarakani hazina kipimo ambapo katika sekta ya Elimu Serikali inatoa Zaidi ya *Bilioni 23* katika mpango wa elimu bure ambapo wilaya ya Arumeru inapata wastani wa shilingi *milioni 600 kwa mwezi*, ambapo pia katika sekta ya afya pamoja na serikali kuendelea kujenga mamia ya vituo vya afya kwa wilaya ya Arumeru serikali imetoa zaidi ya shilingi *Bilioni 1.8* kwa ajili ya ujenzi wa vituo vipya vya afya vya Usa river , Nduruma, Mbuyuni kata ya oljoro pamoja na kituo cha afya cha manyire ambacho kimejengwa kwa ubia na serikali ya Tanzania na Japan ambapo kwa sasa vituo vyote vinafanya kazi uku kituoncha cha afya mbuyuni kikiwa katika hatua za mwisho kufunguliwa. Wazee hao wamesema katika sekta ya afya kwa sasa wilaya inapata wastani wa *shilingi bilioni 1* kwa ajili ya dawa na vifaa tiba kila mwaka ambapo katika halmashauri ya Meru serikali inatoa zaidi ya *milioni 500* pamoja na Halmashauri ya Arusha serikali inatoa *milioni 500* pia katika madawa na vifaa tiba. Katika tukio lingine la kufurahisha wazee hao wamesema katika sekta ya maji serikali imezindua mradi mkubwa wa maji wa shilingi *bilioni 520* ambapo katika mradi huo jumla ya kata 14 zitanufaika na mradi huo wa maji sambasamba na mradi mwingine wa kuondoa fluoride kwenye maji ambapo jumla ya shilingi *bilioni 8* zimetolewa kwa ajili ya kugharamia mradi huo utakaosaidia kaya zaidi ya elfu 50 kupata maji safi na salama Wakihitimisha kongamano hilo wazee *wamemshukuru* Mhe Rais Magufuli kwa kuwajengea barabara kubwa za lami ya njia nne ya *sakina tengeru*, pamoja na *barabara ya By Pass tengeru mpaka ngaramtoni* ambazo zimegharimu zaidi ya *bilioni 360* ambazo kwa sasa zinatumika. Wazee wa Arumeru kwa sasa wameingizwa kwenye mpango wa *kupewa matibabu bure* kupitia mpango wa wilaya kupitia halmashauri kutoa matibabu bure kwa wazee. *Tazama Video clip 3 za wazee wakizungumza pamoja na still pictures za matukio ya kongamano* πŸ‘‡πŸΎπŸ‘‡πŸΎπŸ‘‡πŸΎ *Imetolewa na Baraza la wazee Wilaya ya Arumeru * *28/07/2019*

0

0
Eric Gabriel
Subscribers
8.9K
Total Post
200
Total Views
83.6K
Avg. Views
0.9K
View Profile
This video was published on 2019-07-29 18:22:02 GMT by @Eric-Gabriel on Youtube. Eric Gabriel has total 8.9K subscribers on Youtube and has a total of 200 video.This video has received 0 Likes which are lower than the average likes that Eric Gabriel gets . @Eric-Gabriel receives an average views of 0.9K per video on Youtube.This video has received 0 comments which are lower than the average comments that Eric Gabriel gets . Overall the views for this video was lower than the average for the profile.

Other post by @Eric Gabriel