×

Geah Habibu's video: WAZIRI MKUU AAGIZA UCHUNGUZI ZAIDI UFANYIKE KISA CHA BINTI KUPOTEA SHULENI MBEYA

@WAZIRI MKUU AAGIZA UCHUNGUZI ZAIDI UFANYIKE KISA CHA BINTI KUPOTEA SHULENI MBEYA
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemuagiza Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Juma Homera na Kamati ya Usalama ya Mkoa huo wafanye uchunguzi zaidi na kwa haraka kuhusiana na tukio la kupotea kwa binti Esther Noah Mwanyiru ambaye alikuwa akisoma shule ya sekondari ya Panda Hill mkoani humo. Waziri Mkuu ametoa agizo hilo leo (Alhamisi, Juni 22, 2023) baada ya kupokea clip yenye maelezo ya mzazi wa binti huyo ambaye alikuwa akisoma kidato cha tano, tahsusi ya PCB kwenye shule hiyo. Katika clip hiyo, Mama yake Esther anadai kwamba yeye na mume wake waliitwa na uongozi wa shule hiyo na kujulishwa kwamba Esther hajaonekana tangu asubuhi ya tarehe 18 Mei, 2023 na kwamba hadi sasa zimepita siku zaidi ya 20 wamekuwa wakimtafuta binti yao kila mahali lakini hakuna dalili za kumpata. Mama Esther anadai kuwa Esther aliacha ujumbe wa maandishi akiwaaga rafiki zake na kuomba Mwalimu Jimmy aache kuwafanyia wanafunzi wengine kitendo alichomfayia yeye kwani kimesababisha maisha yake kuwa magumu. “Naomba umfikishie salamu Mwalimu Jimmy, mwambie ameyafanya maisha yangu kuwa magumu sana hapa shuleni. Asiendelee kuwafanyia wanafunzi wengine kama alivyoyafanya maisha yangu mimi kuwa magumu,” alisema mama yake Esther akisoma sehemu ya ujumbe huo.

19

10
Geah Habibu
Subscribers
367K
Total Post
1.3K
Total Views
2.3M
Avg. Views
22K
View Profile
This video was published on 2023-06-23 14:08:28 GMT by @Geah-Habibu on Youtube. Geah Habibu has total 367K subscribers on Youtube and has a total of 1.3K video.This video has received 19 Likes which are lower than the average likes that Geah Habibu gets . @Geah-Habibu receives an average views of 22K per video on Youtube.This video has received 10 comments which are lower than the average comments that Geah Habibu gets . Overall the views for this video was lower than the average for the profile.

Other post by @Geah Habibu