×

Habari za UN's video: Utu Gaza Nani kakubali na nani kapinga

@Utu Gaza; Nani kakubali na nani kapinga?
The Hague, Uholanzi makao makuu ya Mahakama ya Kimataifa ya Haki, ICJ majaji 17 wanaingia ukumbini tayari kutoa uamuzi kuhusu shauri la Afrika Kusini dhidi ya Israel ikitaka mahakama ichukue hatua za awali ili Israel izuie vitendo vya mauaji ya kimbari dhidi ya wapalestina Gaza. ICJ imetangaza hatua 6 za awali ambapo kila hatua ilipigiwa kura na majaji hao 17 ambapo wawili ni wa muda. Mmoja kutoka Afrika Kusini na mmoja kutoka Israel. Miongoni mwa hatua hizo zilizosomwa na Rais wa ICJ Jaji Joan Donoghue ni misaada ya kibinadamu na mahitaji ya msingi kwa wakazi wa Gaza na matokeo ya kura: “Kwa kura 16 dhidi ya 1, serikali ya Israel ichukue haraka mikakati fanisi ya kuwezesha utoaji haraka wa huduma za msingi zinazohitajika na misaada ya kiutu ili kushughulikia mazingira mabaya ya maisha yanayokumba wapalestina Ukanda wa Gaza.” Waliounga Mkono: Rais Donoghue; Makamu Rais Gevorgian; Majaji; Tomka, Abraham, Bennouna, Yusuf, Xue, Bhandari, Robinson, Salam, Iwasawa, Nolte, Charlesworth, Brant; na jaji wa muda Barak na Moseneke. Waliopinga: Jaji Sebutinde.

4

0
Habari za UN
Subscribers
46.9K
Total Post
3.1K
Total Views
70.5K
Avg. Views
592.3
View Profile
This video was published on 2024-01-27 04:22:48 GMT by @Habari-za-UN on Youtube. Habari za UN has total 46.9K subscribers on Youtube and has a total of 3.1K video.This video has received 4 Likes which are lower than the average likes that Habari za UN gets . @Habari-za-UN receives an average views of 592.3 per video on Youtube.This video has received 0 comments which are lower than the average comments that Habari za UN gets . Overall the views for this video was lower than the average for the profile.Habari za UN #HabarizaUN #Gaza #Israel #Palestine The has been used frequently in this Post.

Other post by @Habari za UN