×

Habari za UN's video: Tunawapatia dola milioni 3

@Tunawapatia dola milioni 3!
Vita inayoendelea nchini Sudan mbali ya kukatili uhai wa mamia ya watu imesambaratisha na kupindua maisha ya mamilioni ya watu ikiwa ni pamoja na kuathiri huduma za msingi kama vile chakula, malazi, afya na elimu. Mashirika mbalimbali ya Umoja wa Mataifa yanahaha kukidhi mahitaji ya dharura ya maelfu ya wakimbizi ndani na nje ya Sudan. Asilimia kubwa ya waathirika ni wanawake na watoto ambao sasa mustakabali wao uko njia panda kwani elimu yao imekatizwa na vita hiyo. Kwa kutambua umuhimu wa elimu yao hata wakiwa ukimbizini mfuko wa kimatifa wa elimu haiwezi kusubiri ECW unashikamana na mashirika hayo kusaidia kunusuru elimu ya watoto hao kutoka Sudan. Juma hili ECW, imetangaza kuchagia dola milioni 3 kwa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR ili ziwasaidie watoto wakimbizi wa Sudan walioko nchini Chad kuweza kupata elimu ya dharura. Makala hii iliyoandaliwa na Flora Nducha inafafanua zaidi

1

0
Habari za UN
Subscribers
46.9K
Total Post
3.1K
Total Views
70.5K
Avg. Views
592.3
View Profile
This video was published on 2023-05-20 01:04:24 GMT by @Habari-za-UN on Youtube. Habari za UN has total 46.9K subscribers on Youtube and has a total of 3.1K video.This video has received 1 Likes which are lower than the average likes that Habari za UN gets . @Habari-za-UN receives an average views of 592.3 per video on Youtube.This video has received 0 comments which are lower than the average comments that Habari za UN gets . Overall the views for this video was lower than the average for the profile.Habari za UN #HabarizaUN #UmojawaMataifa #Kiswahili #UNNewsKiswahili #HabarizaUN #UmojawaMataifa #Kiswahili #UNNewsKiswahili Vita has been used frequently in this Post.

Other post by @Habari za UN