×

Habari za UN's video: Habari za UN

@Habari za UN
Mapigano makali yanaendelea nchini Sudan huku shaka na shuku kuhusu njaa kali vikiwa dhahiri kila uchao. Raia wanahaha kusaka usalama na wanakabiliwa na machungu yasababishwayo na vita. Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniain, (WFP) limesema kwamba linatarajia zaidi ya watu milioni mbili kukabiliwa na baa la njaa kwa sababu mapigano yaliyoibuka tarehe 15 mwezi Aprili kati ya majeshi kinzani nchini Sudan. Sudan, taifa la tatu kwa ukubwa barani Afrika likiwa na idadi ya watu takribani milioni 48, kwa kiasi kikubwa linategemea misaada ya kibinadamu. Ni takribani mwezi mmoja, mamia ya watu wameuawa, zaidi ya 150,000 wamekimbia Sudan, na mamia ya maelfu wamekimbia makazi yao, kuongezeka wale ambao tayari walifurushwa kutokana na mizozo ya awali. Kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumi wakimbizi, (UNHCR) wakimbizi hawa wapya wamesaka hifadhi kwenye kambi za wakimbizi zilizo maeneo ya ndani zaidi ya mashariki na kusini mwa nchi, na hivyo kuibua changamoto mpya za kibinadamu. WFP imefikishikia zaidi ya watu 35,000 msaada wa chakula. Msaada huo wa kuokoa maisha kwa walio hatarini zaidi, zikiwemo familia, ambazo hivi karibuni zimekimbia mapigano, wakimbizi waliokuweko Sudan na wakimbizi wa ndani na wenyeji wao wanaowahifadhi. Kwa ujumla, WFP inalenga kusaidia watu milioni 4.9 walio hatarini kwenye maeneo ambako hali ya usalama inaruhusu, halikadhalika “kuzuia na kutibu utapiamlo uliokithiri” kwa watoto 600,000 wenye umri wa chini ya miaka mitano na wajawazito na wanawake wanaonyonyesha watoto. Mkuu wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa inayohusika na misaada ya kibinadamu amesisitiza umuhimu wa sitisho la mapigano la kiutu na kutokomeza ukiukwaji wa haki za binadamu.

2

0
Habari za UN
Subscribers
46.9K
Total Post
3.1K
Total Views
70.5K
Avg. Views
592.3
View Profile
This video was published on 2023-05-13 12:31:40 GMT by @Habari-za-UN on Youtube. Habari za UN has total 46.9K subscribers on Youtube and has a total of 3.1K video.This video has received 2 Likes which are lower than the average likes that Habari za UN gets . @Habari-za-UN receives an average views of 592.3 per video on Youtube.This video has received 0 comments which are lower than the average comments that Habari za UN gets . Overall the views for this video was lower than the average for the profile.Habari za UN #HabarizaUN #UmojawaMataifa #Kiswahili #UNNewsKiswahili Mapigano has been used frequently in this Post.

Other post by @Habari za UN