×

KTV TZ ONLINE's video: RAIS MWINYI AZINDUA BANDARI MPYA ZANZIBAR l HII APA BANDARI KAVU

@RAIS MWINYI AZINDUA BANDARI MPYA ZANZIBAR l HII APA BANDARI KAVU
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi, amesema Mapinduzi makubwa katika sekta ya Miundombinu ya Bandari yanalenga kuifanya Zanzibar kuwa kituo muhimu cha Usafirishaji na kupokea Meli kubwa zinazoleta bidhaa nchini. Rais Dk. Mwinyi ametoa tamko hilo leo tarehe 18 Oktoba alipoifungua Bandari kavu ya Maruhubi, Mkoa wa Mjini Magharibi. Amefahamisha kuwa ufunguzi wa Bandari kavu ni hatua muhimu ya kuimarisha utendaji wa bandari kwani itapunguza msongamano wa makontena katika Bandari ya Malindi. Rais Dk. Mwinyi ameeleza, mabadiliko hayo ya Miundombinu ya Bandari yataleta msukumo mkubwa wa ukuaji wa Uchumi wa Zanzibar na kuwasisitiza wadau kuunga mkono juhudi hizo. Ameeleza kuwa kampuni ya Africa Global Logistic inayoendesha bandari ya Malindi hivi sasa inaendelea kuleta mabadiliko makubwa ya kiutendaji yanayoongeza Ufanisi na kuwapa urahisi Wafanyabiashara kutekeleza wajibu wao bila usumbufu pamoja na kuokoa muda. Dk. Mwinyi amewahakikishia wadau kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, itaendelea kufanya kazi zaidi na sekta binafsi kwani mbali ya kuja na mitaji, pia wanakuja na utaalamu na teknolojia za kisiasa zinazochochea ufanisi kwenye utendaji. Rais Dk. Mwinyi amesisitiza kuwa Serikali ianendelea na Ujenzi wa Bandari Jumuishi ya Mangapwani kwa kuifanya kuwa yenye uwezo wa kuhudumia meli nyingi zaidi ikwemo kampuni za kimataifa kuleta meli za mafuta kwenye bandari hiyo. Amesisitiza, bado kuna fursa zaidi za kuongeza kasi ya utoaji wa huduma kwa bandari zote na kuziagiza taasisi za TRA, ZBS, ZFDA, taasisi ya Atomic energy, na Mkemia Mkuu wa Serikali kuongeza kasi na ufanisi katika utendaji wao ili kuwarahisishia Wafanyabiashara mazingira bora ya ufanyaji wa biashara yatakayopunguza gharama na kumpa unafuu mtumiaji. ....................................................................... Angalia Video Hii Mwanzo mwisho , Kisha Subscribe ili uendelee Kupata Habari Zote. Follow Ktv Tz Online Facebook | KTV TZ ONLINE INSTAGRAM |@ktv_tz_online Wasiliana nasi kupitia number +255 717 619 834 Ktv Tz Online Journalists cc: Sadia Rashid cc: Sauti Byego Camera Department" Dadi Ali Omar (OJ) Nassor Shaibu Abdallah Juma Editors: Juma Maulid Dadi Ali Video Zingine: Angalia hapa - Diamond Platnumz Alivyolisha watoto yatima - Ali Kiba akiwa Oman https://www.youtube.com/watch?v=QQjaQ7ey9Pg https://www.youtube.com/watch?v=Mscbg7grm9Y

60

32
KTV TZ ONLINE
Subscribers
379K
Total Post
4.7K
Total Views
1.5M
Avg. Views
12.1K
View Profile
This video was published on 2024-10-18 18:33:01 GMT by @KTV-TZ-ONLINE on Youtube. KTV TZ ONLINE has total 379K subscribers on Youtube and has a total of 4.7K video.This video has received 60 Likes which are higher than the average likes that KTV TZ ONLINE gets . @KTV-TZ-ONLINE receives an average views of 12.1K per video on Youtube.This video has received 32 comments which are higher than the average comments that KTV TZ ONLINE gets . Overall the views for this video was lower than the average for the profile.

Other post by @KTV TZ ONLINE