×

KTV TZ ONLINE's video: MSHINDI WAKISHUA TWENZETU QATAR ALIVYO JISHINDIA ZAWADI KWA ELFU 6 TU

@MSHINDI WAKISHUA TWENZETU QATAR ALIVYO JISHINDIA ZAWADI KWA ELFU 6 TU
Meneja kanda ya mauzo Unguja vijijini wa kampuni ya tigo zantel, mwajuma semkanga, amesema kampuni yao itaendelea kutoa zawadi mbalimbali kwa wateja wao kupitia shindano linaloendelea hivi sasa. Akizungumza na waandishi wa habari, katika hafla ya kumkabidhi mshindi wa shindano la wakishua kwenzetu Qatari na Hisense, aliyejishindi vitu vya ndani ikiwa ni muendelezo w a kuwapatia zawadi mbalimbali wateja wao hafla ambayo ilifanyika katika duka la Tigo Zantel lililopo Vuga. Alisema mteja wao Omar Ali aliyejishindia vitu mbalimbali ikiwemo TV na Frij kutokana na kufanya miamala katika simu yake kupitia mtandao wa tigo katika sim yake. Alisema kampuni yao kwa sasa imekuwa na promoshani hiyo kwa lengo la kuwamahasisha wateja wao kuendelea kutumia mtandao wao sambamba na kuwawezesha kujiajiri kupitia vitu wanavyopatiwa. Aidha alisema kampuni hiyo itaendelea kuthamini wateja wao na kuwapatia zawadi mbalimbali sambamba na kuahidi kuboresha huduma wanazozitoa kila siku. Alisema mshindi huyo alipatikana kutokana na kufanya miamala mbalimbali kupitia sim yake ya mkononi ambapo ushindi huo aliupata kupitia kutuma fedha. “Mshindi wetu wa leo tumempata ni Omar ambapo mara ya mwisho alitumia huduma ya tigo pesa na aliibuka mshindi wa shindano hili” alisema. Hivyo, aliwataka wateja wa Tigo Zantel kuendelea kutumia mtandao huo kwa kufanya miamala mbalimbali kwa simu ili kujiweka katika nafasi ya ushindi. Nae, Mshindi wa shindano hilo, Omar Ali, alisema, amekuwa akitumia miamala mara kwa mara katika simu yake ikiwemo kununua vocha, umeme pamoja na kufanya miamala ya sim kwa watu mbalimbali. Aidha alisema siri ya kupata ushindi huo ni kufanya miamala kupitia sim yake ya mkononi, hivyo, aliwataka wananchi wanaotumia huduma za mtandao huo kuendelea kutumia huduma zinazopatikana katika kampuni hiyo ili kuweza kuibuka na ushindi. ‘Jana jioni baada ya kutuma fedha tu niliona sim yangu imepigwa kupokea nilijuilishwa kuwa nimeshinda kwenye shindano la shindano la wakishua twenzetu Qatari na Hisense kwa kweli nilifurahi sana kwa kweli shindano hili lipo kweli hivyo watumiaji wa mtandao huu tutumieni fursa hii” alisema. Angalia Video Hii Mwanzo mwisho , Kisha Subscribe ili uendelee Kupata Habari Zote. Follow Ktv Tz Online Facebook | KTV TZ ONLINE INSTAGRAM |@ktv_tz_online Wasiliana nasi kupitia number +255 625 323 932 Ktv Tz Online Journalists cc: Sadia Rashid cc: Sauti Byego Camera Department" Dadi Ali Omar (OJ) Nassor Shaibu Abdallah Juma Editors: Juma Maulid Dadi Ali Video Zingine: Angalia hapa - Diamond Platnumz Alivyolisha watoto yatima - Ali Kiba akiwa Oman https://www.youtube.com/watch?v=QQjaQ7ey9Pg https://www.youtube.com/watch?v=Mscbg7grm9Y

7

3
KTV TZ ONLINE
Subscribers
379K
Total Post
4.7K
Total Views
1.5M
Avg. Views
12.1K
View Profile
This video was published on 2022-10-22 03:39:56 GMT by @KTV-TZ-ONLINE on Youtube. KTV TZ ONLINE has total 379K subscribers on Youtube and has a total of 4.7K video.This video has received 7 Likes which are lower than the average likes that KTV TZ ONLINE gets . @KTV-TZ-ONLINE receives an average views of 12.1K per video on Youtube.This video has received 3 comments which are lower than the average comments that KTV TZ ONLINE gets . Overall the views for this video was lower than the average for the profile.

Other post by @KTV TZ ONLINE