×

KTV TZ ONLINE's video: RAIS MWINYI AFUNGUA BARABARA LAKINI AMEONESHA KUCHUKIZWA NA TABIA HIZI l ATOA MAAGIZO

@RAIS MWINYI AFUNGUA BARABARA LAKINI AMEONESHA KUCHUKIZWA NA TABIA HIZI l ATOA MAAGIZO
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi, ameiagiza Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi kusimamia hifadhi za barabara kwa nguvu zote ili kuzuia wananchi kujenga au kufanya biashara kwenye maeneo hayo. Hatua hii inalenga kuepusha mzigo mkubwa wa fidia kwa serikali inapohitaji kupitisha miundombinu mingine muhimu. Dk. Mwinyi amesema kumekuwepo na tabia ya baadhi ya wananchi kutumia hifadhi za barabara kiholela, hali inayohatarisha barabara zilizopo na kuathiri juhudi za kuboresha miundombinu. Akizungumza wakati akifungua barabara mpya ya Jozani–Charawe–Ukongoroni–Bwejuu yenye urefu wa kilomita 24.5, Rais Mwinyi amesisitiza kuwa wananchi wanapaswa kutunza barabara zilizojengwa na kuthamini jitihada za Serikali katika kuboresha usafiri na kuondoa usumbufu wa awali. Aidha, amewahakikishia wananchi kuwa serikali itaendelea na ujenzi wa barabara bora kote nchini, huku akiwataka kushirikiana katika juhudi hizo. Rais Mwinyi pia amethibitisha kuwa barabara ya **Tunguu – Makunduchi** itakamilishwa kwa kiwango cha njia nne zenye taa, kuanzia Mwanakwerekwe hadi Makunduchi. Angalia Video Hii Mwanzo mwisho , Kisha Subscribe ili uendelee Kupata Habari Zote. Follow Ktv Tz Online Facebook | KTV TZ ONLINE INSTAGRAM |@ktv_tz_online Wasiliana nasi kupitia number +255 717 619 834 Ktv Tz Online Journalists cc: Sadia Rashid cc: Sauti Byego Camera Department" Dadi Ali Omar (OJ) Nassor Shaibu Abdallah Juma Editors: Juma Maulid Dadi Ali Video Zingine: Angalia hapa - Diamond Platnumz Alivyolisha watoto yatima - Ali Kiba akiwa Oman https://www.youtube.com/watch?v=QQjaQ7ey9Pg https://www.youtube.com/watch?v=Mscbg7grm9Y

72

28
KTV TZ ONLINE
Subscribers
379K
Total Post
4.7K
Total Views
1.5M
Avg. Views
12.1K
View Profile
This video was published on 2024-10-24 21:51:46 GMT by @KTV-TZ-ONLINE on Youtube. KTV TZ ONLINE has total 379K subscribers on Youtube and has a total of 4.7K video.This video has received 72 Likes which are higher than the average likes that KTV TZ ONLINE gets . @KTV-TZ-ONLINE receives an average views of 12.1K per video on Youtube.This video has received 28 comments which are lower than the average comments that KTV TZ ONLINE gets . Overall the views for this video was lower than the average for the profile.KTV TZ ONLINE #Zanzibar #UjenziNaMaendeleo #Barabara Angalia has been used frequently in this Post.

Other post by @KTV TZ ONLINE