×

MAELEZO TV's video: Dkt Abbasi Mchengerwa Kumpokea Balozi wa Amani Duniani Keshokutwa anakuja kuunga Mkono Royal Tour

@Dkt. Abbasi, Mchengerwa Kumpokea Balozi wa Amani Duniani Keshokutwa, anakuja kuunga Mkono Royal Tour
Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Hassan Abbasi amesema, Agosti 23, 2022, Tanzania inatarajia kuwa mwenyeji wa ujio wa Balozi wa Amani Duniani na Kiongozi wa kidini kutoka Nchini India Bw. Gurudev Sri Sri Ravi Shankar ambaye atawasili nchini akiwa na ujumbe wa watu 15, na atakuwepo hadi Agosti 27 mwaka huu. Amesema pia jioni ya siku hiyo hiyo, Bw. Gurudev anatarajiwa kuendesha Tamasha kubwa la utamaduni katika ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC) na burudani za kiutamaduni za vikundi vya ngoma kutoka Tanzania na India vitatumbuiza ambapo pia atapata fursa ya kutoa mhadhara kwa Watanzania pamoja na kuendesha zoezi la mtindo wa kuvuta pumzi unaoleta furaha na amani. Mgeni rasmi katika tukio hilo ni Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Mohamed Omar Mchengerwa. Akizungumza na Waandishi wa Habari Jijini Dar es Salaam, Dkt Abbasi amesema Wizara yake kwa kushirikiana na Ubalozi wa India ndio wanaoratibu ujio huo ambao unalenga kuunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Mama yetu Samia Suluhu Hassan za kulitangaza Taifa letu kupitia Royal Tour Amesema Bw. Gurudev Sri Sri Ravi Shankar ni miongoni mwa watu wenye ushawishi mkubwa kutokana na karama aliyonayo ya kuhuburi amani na upendo, ustawi kwa jamii, kuishi maisha ya furaha, kuepuka migogoro, kuwa na uhuru wa mawazo, na kuona kuwa dunia ni familia ambayo kila mmoja ni wa thamani. Aidha amebainisha kuwa ujio wa Gurudev ni wa muhimu kwa kuitangaza nchi ya Tanzania kwani kila mahali anapokuwa, hufuatiliwa na mamilioni ya watu duniani kote na pia moja ya mchango wa kipekee kwa dunia anaoutoa ni mbinu imara ya upumiaji inayowezesha ustawi wa kimwili, kiakili, kihisia na kijamii ambapo tayari amebuni kozi 57 za kuifanya jamii Duniani kuwa na tabasamu, kuepukana na msongo wa mawazo na vurugu. “Katika ziara yake ya Royal Tour nchini Tanzania Bw. Gurudev anatarajiwa kuendesha Tamasha kubwa la utamaduni katika ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC) kuanzia saa 11:30 jioni ambapo burudani za kiutamaduni za vikundi vya ngoma kutoka Tanzania na India vitatumbuiza. Bw. Gurudev atapata fursa ya kutoa mhadhara kwa Watanzania pamoja na kuendesha zoezi la mtindo wa kuvuta pumzi unaoleta furaha na Amani” amesema Dkt Abbasi.

2

0
MAELEZO TV
Subscribers
20.2K
Total Post
5.2K
Total Views
18.3K
Avg. Views
88.9
View Profile
This video was published on 2022-08-23 18:48:07 GMT by @MAELEZO-TV on Youtube. MAELEZO TV has total 20.2K subscribers on Youtube and has a total of 5.2K video.This video has received 2 Likes which are higher than the average likes that MAELEZO TV gets . @MAELEZO-TV receives an average views of 88.9 per video on Youtube.This video has received 0 comments which are lower than the average comments that MAELEZO TV gets . Overall the views for this video was lower than the average for the profile.

Other post by @MAELEZO TV