×

Mringo Tv's video: Rais Magufuli Nitaruhusu Ligi Kuu iendelee Corona ipo ila TUSIOGOPE Tunaweza kuishi nayo

@Rais Magufuli Nitaruhusu Ligi Kuu iendelee |Corona ipo ila TUSIOGOPE | Tunaweza kuishi nayo
RAIS Dk John Magufuli 'JPM' amesema anatamani kuona Ligi Kuu Bara ikiendelea, baada ya kusitishwa kutokana na janga la virusi vya corona vinavyosababisha ugonjwa wa Covid-19. Hata hivyo, JPM amesema anasubiri ushauri wa wataalamu wake kabla ya kuona ligi ikichezwa na kufuatiliwa na mashabiki kupitia televisheni, kwani amebaini katika waathirika wa covid 19 hakuna mwanamichezo yeyote aliyedhurika zaidi, ikionyesha wafanyao mazoezi wapo salama. Rais ametoa kauli hiyo leo Jumapili, alipokuwa akimuapisha Dk Mwigulu Nchemba kuwa Waziri wa Katiba na Sheria, kuchukua nafasi ya marehemu, Balozi Augustine Mahiga aliyefariki dunia Mei Mosi jijini Dodoma. Katika hotuba yake, Rais Magufuli amesema atazungumza na washauri wake kuangalia namna bora ya kurejesha michezo tena, ili ikiwezekana ligi ichezwe na mashabiki kufuatilia mechi hizo majumbani kupitia runinga na njia nyingine za kisasa. Kwa hapa nchini mpaka sasa haijaripotiwa mwanamichezo aliyeambukizwa corona, tofauti na mataifa mengine duniani ambapo nyota kadhaa wa soka Ulaya na wakali wa mchezo wa kikapu wa Ligi ya NBA wamegundulika kuugua ugonjwa huo na kupona. Wachezaji watatu wa klabu ya Juventus inayoshiriki Ligi Kuu ya Italia, Paul Dybala, Daniel Rugani na Blaise Matuidi walikutwa na virusi vya corona, mbali na wakali wengine wa klabu kadhaa za Ulaya ikiwamo Hispania na Ujerumani sambamba klabu kadhaa za NBA. “Ningependa kuona ligi ikiendelea watu watazame mpira, tusitishane kupita kiasi ni kweli ugonjwa upo tuendelee kuchukua tahadhari,” amesema Rais JPM. Alisema ugonjwa wanamichezo wana nafasi kubwa ya kukabiliana na maambuzi ya ugonjwa wa Covid-19, hivyo angependa kuona ligi ikianza ili wapate fursa ya kucheza. “Nitazungumza na washauri wangu kuangalia kama ligi inaweza kuanza ili watu wacheze kwani unapofanya mazoezi ni vigumu kupata ugonjwa huu, angalia hadi sasa hakuna mchezaji aliyeathiriwa zaidi kwa corona, kuonyesha corona inawakwepa wafanya mazoezi,” ameongeza. Shughuli za michezo na burudani ilisimama tangu Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alipotangaza marufuku ya mikusanyiko Machi 17 na kurudia tena Aprili 14 na kuifanya Ligi Kuu Bara inayoongozwa na Simba yenye alama 71 kusimama ikisaliwa na mechi za raundi 10 kumaliza msimu wa 2019-2020. Takwimu za ugonjwa huo mpaka mchana huu kwa mujibu wa tovuti ya Worldometer ni kwamba Tanzania kuna maambukizo 480 na vifo vya watu 16 huku wangine 160 wakipona corona iliyowaambukiza zaidi ya 3.4 milioni duniani kote na kuua watu wasiopungua 240,000. Please Subscribe,like and share my videos THANKS FOR SUPPORTS https://www.instagram.com/mringox2 whatsapp +255 785 990 821

0

2
Mringo Tv
Subscribers
37.4K
Total Post
22
Total Views
615.8K
Avg. Views
3K
View Profile
This video was published on 2020-05-04 12:24:48 GMT by @Mringo-Tv on Youtube. Mringo Tv has total 37.4K subscribers on Youtube and has a total of 22 video.This video has received 0 Likes which are lower than the average likes that Mringo Tv gets . @Mringo-Tv receives an average views of 3K per video on Youtube.This video has received 2 comments which are lower than the average comments that Mringo Tv gets . Overall the views for this video was lower than the average for the profile.

Other post by @Mringo Tv